Thursday, 15 August 2013

SHIRIKA LA TECHNOSERVE LAENDESHA MAFUNZO YA ZAO LA KAKAO WILAYANI KYELA


 Aafisa ugani kutoka kata mbalimbali wilayani kyela
 Shughuli inaendelea
 Vipimo muhimu




Shirika la TECHNOSERVE limetoa mafunzo kwa maafisa ugani wa kata za wilaya ya Kyela,katika ukumbi wa KBC(kyela bussines center) ambapo maafisa ugani wamefundishwa juu ya namna ya kuwa shauri wakulima wa zao la kakao kurekebisha mashamba na uanzishaji wa mashamba mapya,uchaguzi wa mbegu bora na ustawishaji shambani.
Naye mkuu wa mafunzo kutoka shirika la TECHNOSERVE ndugu AZIZI MWILA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa maafisa ugani juu ya kilimo na biashara ya zao la kakao katika Wilaya ya Kyela.
Mariamu Jonas Mlacha afisa ugani kutoka kata ya Ipinda ametoa shukrani kwa Shirika hilo kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo.  Na Upendo Mzumbwe

No comments: