Friday 18 July 2014

MBUNGE JOSEPH MBILINYI "SUGU" AFANYA ZIARA MTAA WA TONYA - ITUHA, JIMBONI MBEYA MJINI



  • APATA FURSA YA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUONGEA NA WAKAZI WA ENEO HILO
  • VIJANA WALIOCHUKUA KADI ZA CCM SIKU CHACHE ZILIZOPITA WAZISALIMISHA 
 Vijana wa Mtaa wa Tonya - Ituha walimpokea Mbunge wao kuelekea Tonya

 Msafara wa Mbunge kuelekea Mtaa wa Tonya

Mbunge alilakiwa na kikundi cha ngoma cha vijana
 
Mbunge Joseph Mbilinyi akicheza ngoma baada ya kuwasili mtaa wa Tonya

 Msafara wa Mbunge ukaelekea kufungua Ofisi ya CHADEMA -Tonya

Mh. Joseph Mbilinyi akiongea kabla ya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Tonya ambaye naye ameshiriki katika kuikamilisha

Hapa Mbunge Sugu akijiandaa kuzindua ofisi

 Akisaini kitabu cha wageni kuonyesha kuwa ofisi imefunguliwa rasmi

 Baada ya zoezi hilo Mbunge alipelekwa na diwani kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa daraja katika mtaa wa Tonya
 Hapo Mbunge Joseph Mbiliyi akiongea na wakazi wanaoishi kandokando ya daraja hilo

 Pia Mbunge alipata fursa ya kutembelea shule ya sekondari ambapo madarasa mapya yamejengwa
Joseph Mbilinyi "Sugu" hapo akiwa katika mkutano wa hadhara katika Mtaa huo wa Tonya

 Wazee nao walikuwepo kusikiliza Mbunge akielezea shuhuli za kimaendeleo zilizofanyika jimboni

 Mmoja wa Kijana maarufu wa eneo hilo ambaye alichukua kadi ya CCM siku chache zilizopita alirudisha kadi  kwa Mbunge na kuelezea kuwa alichukua  kwa  kuwa alikuwa akihitaji shilingi 5,000 zilizokuwa zinagawiwa na CCM kwa vijana ili wagawiwe kadi hizo za CCM
 Wazee wakimshukuru Mbunge kwa kuwa mwakilishi wao mwema katika jimbo la Mbeya mjini

 Vijana wakikabidhiwa kadi za CHADEMA na mbunge wao


 Vijana wakiwemo ambao walirudisha kadi za CCM siku chache zilizopita wakiwa wanaonyesha kadi zao za CHADEMA walizokabidhiwa na Mbunge
 Wananchi wakionge na Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya mkutano wa hadhara

 Baadaye Mbunge Sugu alimalizia na kikao cha ndani na baadhi ya wakazi wa Tonya ambapo pia alipata fursa ya kupokea maoni na maswali na pia alitolea ufafanuzi mambo mbalimbali
Kwa hisani ya 
blog ya Joseph Mbilinyi

No comments: