Thursday 28 August 2014

WAZEE KYELA WAMTAKA MWANYAMAKI KURITHI MIKOBA YA DR,MWAKYEMBE






BAADHI ya wazee kutoka tarafa za unyakyusa na ntebela wilayani Kyela mkoani Mbeya wamemtaka mwenyekiti mtendaji wa asasi ya pambana saidia jamii wilayani humo Abraham Mwanyamaki kujipanga kuchukua mikoba ya mbunge wa jimbo hilo Dr,Harrison Mwakyeme 2015.

Wazee hao walitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati mwenyekiti huyo alipokuwa akitoa misaada ya kijamii katika tarafa hizo kama moja ya kutimiza maombi ya misaada aliyoombwa na wananchi kwa ajili ya kuondokana na changamoto zinazowakabili.

Jakson Mwakanyamale mkazi wa Ntebela alisema kuwa mwenyekiti huyo amesaidia mambo mengi hasa sekta ya elimu,afya,kilimo na kuviwezesha vikundi vya wajasilia mali na kuwa wao kama wazee wa Kyela wanamuhitaji ili awe muwakirishi wao.

Mwakanyamale alisema kuwa wilaya ya Kyela ina wasomi wengi ambao wananyadhfa kubwa serikalini na kwenye sekta binafsi lakini wamekosa uzalendo wakulisaidia jimbo hilo ambalo limekuwa likipoteza sifa siku hadi siku kutokana na kuwa na matatizo lukuki yasiyo tatulika.

Evansi Mwakalyobi mkazi wa Unyakyusa alisema kuwa kazi za kuondoa changamoto za wilaya hiyo zilitakiwa zifanywe na mbunge lakini mbunge wao amewasaliti hivyo wanamuhitaji mwenyekiti huyo kwa kuwa tayari amefanya mambo makubwa na jamii inamtambua.

Alisema kuwa wananchi wanaoingia katika wilaya hiyo wakitokea mikoani wanashikwa na butwaa wanapoliona jimbo hilo likiwa choka mbaya ukilinganisha na jinsi Kyela ilivyo na wasomi wengi ambao wengine wanasifika kwa uchapa kazi lakini wanakotoka kupo hoi.

Mwenyekiti mtendaji wa asasi hiyo Abraham Mwanyamaki ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu Taifa na mlezi wa Chadema wilayani humo alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kama chama chake kitampa ridhaa atafanya hivyo.

Alisema kuwa amekuwa akiulizwa na watu wa kada mbalimbali kuhusu kugombea ubunge katika jimbo hilo pindi anapofanya kazi za kijamii kupitia asasi wakitaka agombee lakini hakuweza kujibu na kuwa kama wazee na wananchi kwa ujumla wataona anafaa basi hata kuwa na kinyongo.

Wilaya ya Kyela ni moja ya wilaya katika mkoa wa mbeya inayosifika kwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato kama zao la kakao,mpunga,mawese na vinginevyo ambavyo vinaingiza pato kubwa huku miradi ya maendeleo ikisuasua mengine ikijengwa chini ya kiwango kutokana na kukosa wasimamizi makini.

No comments: