Tuesday 5 May 2015

Kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na mazingira yaikataa kwa mara ya pili bajeti ya wizara maliasili na utalii.


Kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na mazingira kwa mara nyingine tena imekataa kujadili bajeti ya wizara ya maliasili na utalii kwa madai kuwa wizara hiyo haijatekeleza maelekezo ya bunge yanayolenga kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini na kuongeza mapato ya serikali yanayotakiwa kutumika kwa shughuli za maendeleo ya jamii na taifa.

Akiongea jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya mkutano kati ya wizara na kamati hiyo kuvunjika, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na mazingira James Lembeli amesema wizara imekwenda kinyume na maagizo ya kamati kuhusu kurekebisha mipaka ya hifadhi ya taifa ya sadani na hifadhi ya taifa ya ruaha kinyemelea bila kufuata taratibu za kisheria na pia kuchelewa kuridhia viwango vya tozo za utalii kwa shirika la hifadhi za taifa Tanzania TANAPA na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro utaratibu ambao unaikosesha serikali fedha nyingi mpango ambao amesema usipodhibitiwa utaua uhifadhi ambao umekuwa na mchango mkubwa kwa pato la taifa.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Mary Mwanjelwa na Grace Kiwelu wamesema uamuzi wa kukataa kujadili bajeti hiyo umefikiwa na wajumbe wote wa kamati hiyo na umezingatia maslahi ya taifa bila kujali itikadi za vyama na kwamba wizara ya maliasili na utalii sasa imetakiwa kupeleka maelezo ya kuridhisha mjini dodoma mei 14 mwaka huu vinginevyo hawatakuwa tayari kujadili wala kuipitisha bajeti ya wizara hiyo.
Akiongea kuhusu mgogoro huo ambao umesababisha bajeti ya wizara yake kushindwa kujadiliwa na kamati chini ya utaratibu wa kawaida,waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amesema serikali imepokea maelekezo ya kamati baada ya kuomba ipewe muda wa kuandaa majibu ambayo sasa yatawasilishwa mbele ya kamati mjini dodoma wiki ijayo.

No comments: