Serikali imeagiza wananchi wote ambao wamejenga nyumba kuzunguka mgodi wa North Mara kuzibomoa mara moja nyumba hizo kabla ya serikali haijachukua hatua.
Serikali imeagiza wananchi wote ambao wamejenga nyumba kuzunguka mgodi wa North Mara baada tu ya kufanyika kwa tathimini ya mwaka 2011 kwa lengo la kutaka kulipwa fidia na mwekezaji kampuni ya ACACIA MINING kuzibomoa mara moja nyumba hizo kabla ya serikali haijachukua hatua ya kubomoa ili kutokwamisha mipango mbalimbali ya uendeshaji wa mgodi huo.
Agizo hilo la serikali limetolewa na naibu waziri wa nishati na madini anayeshughulika sekta ya madini Mh.Charles Kitwanga,baada ya kutembele baadhi ya vijiji na kushuhudia maefu ya nyumba maarufu kama tegesha ambazo zimejengwa ndani ya miezi mitatu tu baada ya zaoezi la tathimini kukamilika kwa lengo la kutaka kulipwa fidia kubwa,ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi le ambao tayari wamefanyiwa tathimini kupokea fidia yao na kupisha katika maeneo hayo.
Akito maelezo kwa naibu waziri huyo wa nishati na madini,meneja uendelezaji wa mgodi wa North Mara Bw. Abel Yiga,amesema awali walikusudia kuufunga mgodi huo kutokana na changamoto hiyo ya uvamizi wa maeneo hayo baada ya tathimini ya mwaka 2011 kuonyesha kuwa kiasi cha shilingi bilioni tano kilitajika kulipwa kama fidia lakini baada ya ujenzi huo kufanywa kinyume na taratibu inahitaji kiasi cha shilingi bilioni 40 ili kulipa fidia hiyo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji hivyo,wamekiri kuwa tatizo la umasikini ni moja ya sababu ambayo iliwafanya kujenga majengo hayo lengo la kushawishi kulipwa fidia kubwa hivyo wameiomba serikali na uongozi wa mgodi kukubali kutoa fidia kwa wananchi wanaomiliki maeneo hayo kabla ya kufanyika zoezi la tathimini ya mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment