Tuesday, 5 May 2015

Waziri mkuu Mh.Pinda amesema serikali imejipangakuongeza idadi ya wanafunzi wanaosomea fani ya uuguzi na ukunga.


Waziri mkuu wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Mh.Mizengo Peter Pinda,amesema  kuwa  serikali ya Tanzania imejipanga kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosomea fani ya uuguzi na  ukunga ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na  zahanati kwa kila kijiji na kata kama moja mkakati wake wa kupunguza vifo vya wanawake    wajawazito na watoto wachanga.

Waziri mkuu Pinda ameyasema hayo mkoani mara wakati akihutubia mamia ya wananchi katika  viwanja vya shule ya msingi ya mkendo mjini musoma katika maadhimisho ya siku ya wakunga  duniani,kwani amesema katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 imeonyesha kuwa kati   vizazi hai laki moja,wanawake 432 wamekuwa wakifariki dunia kila mwaka kwa matatizo mbalimbali wakati wa kujifungua.
 
Kwa sababu hiyo waziri amezita halmashari zote nchini kutoa kipaumbele katika kuwapatia  wakunga nafasi ili waweze kutoa mchango wao katika kupunguza vifo vya wanawake  wajawazito na watoto.
 
Kwa upande wake naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Mh.Stephen Kebwe,akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya wakunga dunia kitaifa ambayo yamefanyika mjini musoma,amesema tanzania imekuwa miongoni mwa nchi  tano katika bara la afrika kwa kupunguza vifo vya watoto na kuvuka lengo la mellenia tangu mwaka 2012 juhudi ambazo   zimefanywa na wakunga. 

No comments: