Serikali kwa kushirikiana na tume ya mipango imesema baadhi miradi ya maendeleo iliyopo katika vipaumbele vya mpango wa matokeo makubwa sasa imeshindwa kutekelezwa kwa kiwango kilichokusidiwa kutokana na nchni wahisani kukataa kutoa fedha walizoahidi baada ya kuibuka kwa sakata la ESCROW.
Akizungumza na kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti,waziri wa nchi ofisi ya rais mahusiano na uratibu Mhe. Mary Nagu amesema serikali imepanga kuhamasisha mali zilizo katika sekta binafsi nchni zitumike katika mikopo itakayo saidia kuziba pengo la fedha zinazoahidiwa na nchi wa wahisani kwa ajili ya miradi ya maendeleo hapa nchni ili kupunguza utegemezi.
Awali wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wamehoji kukwama kwa miradi iliyopo katika sekta za vipaumbele ikiwemo miradi ya maji vijijini na kusababisha wakandarasi kuanza kudai malipo ya fedha kwa hatua ya miradi ilipofikia baada ya serikali kushindwa kutoa fedha kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano.
Aidha katika kiako hicho kamati ya bajeti imeshtushwa na kuwepo kwa mwekezaji anayateka kuwekeza katika mradi wa za Treni ambaye tayari ameshatembelea katika mikoa mbalimbali kwa muda mrefu bila ya kupata ushirikiano toka serikali na tume ya mipango haina taarifa yeyote kuhusu mwekezaji huo,hatua inayoweza kusababisha mwekezaji huyo kukimbilia nchni jirani.
No comments:
Post a Comment