Monday, 13 July 2015

SIMBA SC YAWA MCHARO...MZIGO WA OKWI UKO NJIANI




Uongozi wa klabu ya Simba umesema unatarajia kupokea pesa yao ya kumuuza mshambuliaji wao Emanuel Okwi muda wowote kuanzia sasa kutoka klabu ya Sonderjyske ya Denmark ambayo Mganda huyo amejiunga nayo siku za hivi karibuni.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema, peasa hiyo wataitumia kusajili wachezaji ambao wataziba pengo lililoachwa na Emanuel Okwi.
“Tayari wameshatuletea barua na tumeshaandika ‘invoice’ na wanasema watatulipa tarehe 17 kiasi cha dola za kimarekani 110,000”, amesema Poppe.
“Pesa hiyo ikiingia tutaitumia kwa matumizi ya klabu mojawapo ikiwa ni kusajili wachezaji wengine mbadala kwaajili ya kuziba pengo lake na mambo mengine kadha wa kadha ambayo tunafikiria yatatusaidia kwenye klabu”, aliongeza.
Kiasi hicho cha pesa kikibadilishwa kwenye pesa za kitanzania (Tsh.) inakuwa ni zaidi ya shilingi milioni 230 za Tanzania.
Emmanuel Okwi alikuwa amebakiza miezi 9 kumaliza mkataba wake ambao ulikuwa unamalizika mwezi April mwaka 2016. Mkataba wa Okwi ulikuwa na kipengele kinachoelekeza kuwa, ikiwa atapata timu nyingine basi uongozi umruhusu aondoke na kwenda kujiunga nayo.

No comments: