Saturday 1 October 2016

Madiwani mkoani Songwe wamekiri wazi kwamba hawajui kutafsiri taarifa za fedha

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi,mkoani Songwe wamekiri wazi kwamba hawajui kutafsiri taarifa za fedha kutokana na kutokuwa na uelewa wa hesabu na kuwa kitendo cha kuwataka wapitishe taarifa hizo ni sawa na kuwataka wabariki jambo ambalo hawana uwezo nalo.

Hayo yalijili jana katika kikao cha dharura cha cha baraza kamili la madiwani cha kufunga hesabu za halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015 unaoishia Juni 30,2016 na kuziwasilisha kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kwa ajili ya ukaguzi septemba 30 kabla ofisi haijafungwa.

Diwani wa kata ya Igamba Exzaud Kibona alisema ni vigumu kupitisha mambo magumu bila kuwapa muda wa kuyapitia na kuwa na uelewa ambao utaleta ufanisi.

"Mumetuletea taarifa ya fedha ili tuipitishe, sijui mlikusudia nini kulifanya jambo hili kuwa la dharura kiasi hiki, kututaka madiwani tupitishe mambo makubwa ya halmashauri yetu kwa muda mfupi" alisema Kibona.

Sebastian kilindu ni diwani kata ya Mlowo alisema wapo hewani kwani hawaelewi cha kufanya na kuhoji kuna ulazima gani wa kuleta kwa dharura jambo hilo, wangepewa muda wa kutosha ili waweze kuhoji kwa manufaa ya halmashauri yao lakini kwa sasa hawana cha kuhoji.

" tunatunabuluzwaahapanaeli utarutaratibuouliowekwakupata taarifa nyetnyeti dakidakikaa ya mwismwishoarutaratibu ubadubadilike kuiekuiepushamashauri yetu na aibuaibukupata hatihatimashKilindua mrefu" alisema Hapa

Naye diwani kata ya Halungu Maarifa Mwashitete(Chadema) alisema kazi ya kufunga hesabu za halmashauri imefikishwa kwao si kwa lengo la kufanyiwa kazi bali ili iidhinishwe na kupewa baraka za baraza la madiwani maana hakuna hata diwani mmoja anayeweza kuijadili.

Mkuu wa wilaya ya Mbozi John Palingo aliungana na madiwani hao kwa kusema kwamba taarifa hiyo imeandaliwa kitaalamu, hivyo kwa mtu asiyekuwa mhasibu hawezi kuielewa hata angepewa muda wa kuisoma, lakini aliwashauri madiwani kuhakikisha watendaji wa halmashauri wanafuata taratibu wakati wote wa utendaji wao na kuwa na nyaraka zote zinazohusiana matumizi ya fedha za umma.

Hata hivyo aliwasihi madiwani kuamini kilichopo kwani yeye kama mhasibu amepitia na ameona hesabu ziko vizuri.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbozi Edina Mwaigomole alisema wamelazimika kuitisha kikao cha dharura kwa vile walikuwa wanafanya kazi ya kuandaa kwa kupita maeneo mbalimbali ya wilaya na kwamba ilikuwa ni lazima iwasilishwe Septemba 30 mwaka huu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri Elick Ambakisye akitoa azimio la kikao hicho alisema kwa vile wajumbe wa baraza lake hawana uelewa wa hesabu, pia hawajapata fursa ya kuipitia wameamua kuipitisha hesabu hizo kwa sharti la kuingia mkataba na watendaji wa halmashauri kusudi iwapo ukaguzi wa (CAG) utatoa hati chafu watawajibika kwa matokeo hayo.

Halmashauri ya wilaya ya Mbozi imekuwa ikipata hati za mashaka katika kipindi cha miaka minne mfululuzo jambo ambalo limezua hofu.
Mwisho

No comments: