Thursday 8 June 2017

HIFADHI YA MSITU WA MLIMA RUNGWE (MOUNT RUNGWE NATURE RESERVE)


Hifadhi ya Msitu wa Mlima Rungwe ilinzishwa kisheria na Serikali ya kikoloni mnamo mwaka 1949, mwaka 2009 msitu huu ulipandishwa hadhi ya uhifadhi wake na kuwa Hifadhi ya mazingira Asilia ya Mlima Rungwe.

Uhifadhi asilia una maana ya kupunguza muingiliano wote wa shughuli za kibinadamu katika Hifadhi na kuacha uasilia wa mahali utegemee mabadiliko ya kiasili tu (non-consumptive type of conservation), kwa sasa msitu huu unasimamiwa na wakala wa misitu Tanzania (TFS)

Hadhi ya Uhifadhi wa Msitu huu kwenda ngazi ya Hifadhi ya Asilia, ulifanywa kupitia Tangazo la serikali, yaani GN No.386 ya mwaka 2009. Hifadhi hii ina ukubwa wa hekta kumi na tatu elfu mia sita hamsini na mbili (13,652) na ni moja kati ya hifadhi za misitu ya Asili kumi na mbili (12) nchini Tanzania.

Hifadhi hii ni makao ya wanyama na mimea mbali mbali (high biodiversity value), aidha, ni chanzo kikubwa cha maji kwa matumizi mbalimbali hususan ni yale yanayojaza Ziwa Nyasa, pia tafiti nyingi tofauti za kisayansi hufanyika mara kwa mara na wadau tofauti wakiongozwa na Shirika la Hifadhi ya wanyamapori na Mazingira (WCS).

Vivutio vya kitalii ndani ya hifadhi ya msitu wa mlima rungwe. Hifadhi hii ina vivutio vingi, baadhi ya viumbe wengine hawapatikani sehemu nyingine isipokuwa katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Mlima Rungwe, mfano wa viumbe hao ni nyani aina ya Kipunji (Rungwecebus kipunji) aliyegunduliwa kwa mara ya kwanza katika Hifadhi hii na Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS) mwaka 2003.

Vivutio vingine sambamba na huyo nyani ni kama vile uwepo wa Mlima wa tatu kwa urefu Tanzania Mlima Rungwe wenye Urefu wa mita elfu mbili mia tisa themanini na moja (2981) maalum kwa wanamazoezi wapanda milima (Mountain Hikers), Maji moto, Mashimo ya volcano Kama vile Paluvalalutali, Lusiba na Ng’ombe ambayo mashimo hayo kwa sasa yamekufa (Dead volcanic craters).

Wanyama wadogo wadogo zaidi ya aina mia tano (500) kama vile Minde (Abbot duiker), chura wekundu, mijus, nyoka wa chi baridi, panya nk pia Aina zaidi ya mia nne (400) za mimea hupatikana ambayo baadhi ya mimea hiyo hutumika kama dawa kwa wakaazi waliozunguka Hifadhi hii.

Je Ungependa kutembelea kuvutio huki? Tafadhali Wasiliana nasi kwa 0783545464 uyolecte@gmail.com

No comments: