Walimu
wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya
sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi
la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha
tatu shuleni hapo.
Akizungumza
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama, January Lugangika amesema waalimu wa wanafunzi hao wamekikuka
maadili ya ualimu na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza
kuwa tabia hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii.
Aidha
mwenyekiti huyo amedai kuwa ushahidi wa tukio hilo umethibitishwa na
Daktari ambaye aliwafanyia vipimo na kuthibitisha ni kweli kitendo hicho
kilifanyika
Kwa
upande wa Afisa elimu wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato
amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda
yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.
"Inabidi
wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini
shuleni na kama mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na
badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita," alisema Singato.
Watuhumiwa wa tukio hilo ni mwalimu Fredriki Shebila na Saddat Mohamed.
No comments:
Post a Comment