Makombora hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido.
Tukio
hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha
katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.
Waziri
mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao
haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.
Hakuna
juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo licha ya hapo
awali kudai kuwa ilikuwa na uwezo huo, na badala yake ilitoa onyo la
kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini.
Wanajeshi wa Marekani na Japan wanafanya zoezi la pamoja katika eneo hilo la Hokkado.
Rais
wa Korea Kusini Moon Jae-in ameagiza uwezo wa utumiaji nguvu ili
kujibu shambulio hilo.Ndege nne za Korea Kusini zilifanya zoezi la
kurusha makombora jana.
Bwana
Abe alisema kuwa amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba
wote wamekubaliana kuiongezea vikwazo Korea Kaskazini.
Katika
mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea
kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi
hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa.
Katika
siku za hivi karibuni, Korea Kaskazini ilijaribu kombora lake
lililopata mafanikio kutokana na uwezo wake wa kuweza kuifikia Marekani
na kuonyoa kuwa inasimamia mipango yake ya kushambulia kwa makombora
eneo la Marekani la Guam, kilomita elfu mbili kusini mashariki mwa
Japan.
No comments:
Post a Comment