Friday 14 July 2017

Okwi kukwea pia kuifuata Simba Sauz


Emmanuel Okwi

MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Uganda, Emmanuel Okwi anatarajia kukifuata kikosi hicho Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya muda mfupi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao akitokea Uganda alipokuwa akiitumikia timu ya taifa.

Simba inatarajia kuondoka nchini Jumatano ijayo kwenda kuweka kambi ya siku chache Afrika Kusini kisha kurejea kujiandaa na safari ya Uturuki.

Okwi amesajiliwa na Simba hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili ambapo kwa sasa bado hajajiunga na timu kutokana na kuwepo katika kikosi cha timu yake ya taifa katika mchezo dhidi ya Sudan Kusini, kesho Jumamosi ukiwa ni wa kufuzu michuano ya Chan.

Taarifa ambazo Championi Ijumaa limezipata kutoka Simba ni kwamba, awali mshambuliaji huyo alitakiwa kutua nchini baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Sudani Kusini, lakini uongozi umeona ni vyema aifuate timu Afrika kusini kuliko kuja Tanzania.

“Okwi atajiunga na timu Afrika kusini baada ya kwenda huko wiki ijayo kwani timu inatarajia kuondoka Jumatano, hivyo uongozi umeona ni vyema aende huko moja kwa moja kuliko kuja huku itakuwa usumbufu,” kilisema chanzo.

No comments: