Watu
wanane wamekufa na wawili wameokolewa wakiwa salama baada ya Toyota
Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri wilayani
Misungwi.
“Kwa sasa uokoaji unaendelea, abiria wawili ndio wametoka salama. Maiti nane zimeopolewa,” amesema Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama.Temesa ndiyo inasimamia kivuko hicho.
Mshama amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.
Amesema
ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo
wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.
No comments:
Post a Comment