Saturday 22 December 2012

MCHUNGAJI APEWA MSOKOTO WA BANGI MAKABURINI, ATIMUA MBIO

MCHUGAJI wa kanisa la aliyejulikana kwa jina ka Mchungaji Msyaliha wa usharika wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, alionja joto la jiwe makaburini baada ya kupewa msokoto wa Bangi na vijana ambao walikuwa wakimzika mwenzao.

Tukio hilo lilitokea wiki hii eneo hilo la Mbalizi katika msiba wa kijana Denis Sanga ambaye alifariki dunia kwa kile kinachoodaiwa kuwa ni ajari iliyosababisha mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

Vijana hao baada ya kumalizi kuchimba kaburi hilo walilazimisha kufunuliwa jeneza la marehemu huyo na kuweka misokoto ya bangi huku wengine wakivuta hadharani huku wakihamasishana mchungaji huyo apewa bangi.

Vijana hao walisikika wakiimba '''Mpe bomba mpe bomba mchungaji hana hasira'' na baadaye ukaletwa msokoto mkubwa wa bangi ili mchungaji huyo akabidhiwe jambo ambalo lilimtia hofu mchungaji huyo kisha kuanza kukimbia na kushindwa kutoa neno la Mungu.

Baada ya kuzika, walitangaza hali ya hatari kwa wafiwa kuwa mahala pale hairuhusiwi mtu kutoa fedha kwa ajili ya Rambirambi maana fedha hizo ndizo zilizosababisha kifo cha mwenzao ambaye Baba yake Frank Sanga ni mfanyabiashara maarufu eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya.

No comments: