Muuguzi mkuu hospitali ya wilaya ya Bunda Adelaida Masige.
MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA STEPHEN WASIRA
ZAHANATI ya Bunda mkoani Mara, inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya chumba cha kuchomea sindano wagonjwa kukosa madirisha.
Hali hiyo
imebainika baada ya waandishi wa habari kutembelea zahanati hiyo na kuzungumza
na uongozi wa zahanati chini ya muuguzi mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bunda
Adelaida Masage.
Msaidizi wa
mganga wa zahanati ya Bunda Victoria Awino alikiri kuwepo kwa hali hiyo na
kusema kuwa hiyo ni moja ya changamoto wanazozipata wataalam waliopo kwenye
zahanati hiyo.
alisema kuwa
katika zahanati hiyo kuna tatizo la miundombinu na kubwa zaidi ni pamoja na
kukosekana na kwa dirisha katika chumba hicho muhimu cha kuchomea sindano
wagonjwa.
‘’Tatizo
kubwa la miundombinu ni pamoja na chumba cha kuchomea sindano wagonjwa kutokuwa
na dirisha na sehemu ya mapokezi pia hatuna dirisha na nyumba za watumishi ni
tatizo’’ alisema Victoria Awino.
Zahanati hiyo
ya Bunda inahudumia wagonjwa kati ya 30 mpaka 40 kwa siku.
No comments:
Post a Comment