Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za
Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao
wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota
Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea
Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza
kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa
kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa
wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi
walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye
magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba
94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za
Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika
maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini
Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao
hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa
zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe
kazi.
No comments:
Post a Comment