Kaimu
kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki
|
HIVI NDIVYO DALADALA HII ILIVYO HARIBIKA BAADA YA AJALI HIYO KUTOKEA
GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE IKIWA IMEGONGANA USO KWA USO NA GARI AINA YA LAND CRUISER
HIZI NI BAADHI YA MAITI ZILIZO OKOLEWA PUNDE BAADA YA AJALI KUTOKEA
MWILI WA DEREVA WA DALADALA ALIYE FARIKI PAPO HAPO UKIPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI RUFAA
******************************
Watu
sita wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya
Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mbeya.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na madereva mmoja wa
Hiace.
Masaki
amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye
kuwa anaendesha Gari nambali T178 AAV aina ya Toyota Hiace inayofanya
kazi Sokomatola na Uyole ambapo muda huo ilikuwa ikitokea Sokomatola
kuelekea uyole.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Maiti
nne hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria
katika Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
jijini Mbeya.
Aidha
amesema majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo
wanawake watano na mwanaume mmoja . Ambao mpaka sasa majina yao
hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa vibaya.
Chanzo
cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi wa Magari hayo na wito
ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za Barabarani ili
kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea. Ikizingatiwa hilo ni eneo la
Jiji.
No comments:
Post a Comment