
Kamati ya
Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo
la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20
mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi
Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.Akitangaza
mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi
zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13
wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
hdg
Fomu kwa
wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi
hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na
kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh.
500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.
Mbwezeleni
amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na
wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada
ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa
kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.
Kwa
upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi
20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.
KAMATI YA SHERIA SASA KUPITIA USAJILI IJUMAA
Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka
huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa klabu
za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza sasa itakutana keshokutwa (Agosti
16 mwaka huu) saa 4 asubuhi.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Alex Mgongolwa amepanga tarehe hiyo mpya baada ya kikao
cha jana kushindwa kupata akidi. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane
wajumbe kuanzia wanne.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment