Mwanafunzi aliyekuwa akisubiri
kufanya mtihani wa kidato cha nne unaotaraji kuanza kesho Bw Khamis
Mkundo mkazi wa Mwangata C katika Manispaa ya Iringa akiwa
amejinyonga usiku huu kuhofu mtihani wa kidato cha nne
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe ulioachwa na marehemu huyu
Askari kanzu akikagua mwili wa mwanafunzi huyo leo
Wananchi wa Mwangata mjini Iringa wakiwa nyumbani kwa marehemu usiku huu
Mwili wa kijana huyo ukitolewa tayari kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Mwili huo ukipakiwa katika gari la polisi |
Mwanafunzi wa aliyekuwa akisoma
shule ya sekondari Sabasaba mjini Iringa akijiandaa kurudia
kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kupitia kituo cha
Krelluu mjini Iringa Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika
manispaa ya Iringa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa kile
alichodai kuchoshwa na kufeli mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.
Katika barua yake ndewfu
aliyoiandika kijana huyo amesema kuwa amefanya hivyo si kwa
kujipendea ila amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara
hiyo kuamua kujiua ili kuepuka na aibu katika mtihani ujao ambao
anaamini angefeli.
Shemeji wa kijana huyo Aden Tagalile
ameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa tukio hilo
limetokea mida ya kati ya saa 12 na saa 1 usiku wa leo baada ya
kuwepo kwa mazungumzo ya muda mrefu kwa kijana huyo kuonyesha
kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi mtihani wa kidato cha nne
bila mafanikio.
Kwani alisema hajapenda kuona anaendelea kufeli na kuwa yupo tayari kwa lolote kukwepa aibu ambayo ipo mbele yake.
Hata hivyo kufuatia mazungumzo hayo
kijana huyo aliangana na ndugu zake akiwemo kaka yake anayeishi nae kwa
kila mmoja kuondoka nyumbani hapo kabla ya kijana huyo kukutwa
amejinyonga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo
Sarehe Mgimwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuonyesha ujumbe
ambao kijana huyo ameuacha .
No comments:
Post a Comment