Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoani Mbeya, limetangaza kiwango
kipya cha mishahara inayotakiwa kuwa kima cha chini ni Sh 750,000.(HD)
Mwenyekiti
wa Tucta mkoani hapa, Alinanuswe Mwakapala alisema kwa maisha ya sasa
kima cha chini lazima kiwe Sh750,000 na kwamba, pendekezo hilo la mkoa
litawasilishwa kwenye ngazi za juu za Tucta ili kulibariki.
Mwakapala
alisema hayo kwenye hafla ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
kukabidhiwa jengo la ghorofa tano lililojengwa na Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT).
"Wafanyakazi
nchini sasa wamechoshwa na mishahara midogo, hivyo wakati umefika kwa
wafanyakazi kutoogopa maandamano na migomo kudai haki," alisema huku
akishangiliwa.
Hata
hivyo, Rais wa CWT, Gratius Mukoba alisema madai ya wafanyakazi
yaliyowasilishwa Serikalini ni kutaka nyongeza ya mishahara kwa asilimia
100.
Mkoba alisema CWT hivi sasa wanasubiru ndani ya miezi mwili hadi Desemba kupata majibu.
hayatapatikana basi Serikali ijue imejipalia mkaa.
''Hatuwezi
kuendelea kuwaona watu wasiofanyakazi wanapata mishahara mikubwa wakati
wafanyakazi wanasota. Mwisho wa matatizo hayo ni sasa'' alisema huku
akiwataka wafanyakazi hususan walimu kuachana na njama za kutaka
kuwatenganisha.
Alisema
Serikali inatakiwa kuwalipa walimu Sh49 bilioni wanazodai zikiwamo Sh30
bilioni walizopunjwa katika mishahara na kwamba pia lazima ipunguze kodi
kwa wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi.CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment