Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi alisema tukio hilo limetokea juzi
katika kijiji cha Bumilayinga, na kumtaja mwanamke aliyeuawa kuwa ni
Maurisia Malangalila (65).Alisema kuwa sababu za mauaji hayo ni imani za
kishirikina.
Kamanda Mungi aliongeza kuwa kutokana na mauaji hayo, jeshi hilo linamtafuta mkazi wa kijiji hicho Patrick Ngerenge
ili achukuliwe hatua za kisheria kwa madai kuwa alikimbia baada ya tukio hilo.
Hata hivyo, Mungi alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa
mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya kutiwa mbaroni.
No comments:
Post a Comment