Bw. Sam Kutessa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum,
New York
Jumuiya
ya Kimataifa inajiaanda kwa mkutano maalum na wa aina yake kufanyika,
ambapo nchi wanachama watakutana na kujadiliana kwa kina kuhusu
changamoto na adhari kubwa zitokanazo na biashara haramu na matumizi ya
dawa za kulevya.
Mapema
wiki iliyopita, wajumbe wanaoziwakilisha nchi zao hapa Umoja wa Mataifa,
walikuwa na mkutano wa siku moja ambao ulikuwa ni sehemu ya maandalizi
ya mkutano huo maalum utakaofanyika mwezi Aprili 2016.
Mkutano
huo wa maandalizi uliofanyika hapa Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na
wadau mbalimbali wakiwamo mawaziri kadhaa kutoka nchi hasa za Amerika ya
Kati ambako nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto kubwa ya biashara
hiyo, uliandaliwa na Bw. Sam Kutessa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa.
Katika
majadiliano ya mkutano huo , ilidhihirika wazi kwamba hakuna nchi hata
moja duniani iwe tajiri au maskini ambayo haijakumbwa na janga la
biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
" Hakuna
nchi ambayo imepona kutokana na biashara hii yenye thamani ya mabilioni
ya dola. Licha ya juhudi kubwa na raslimali nyingi ambazo mataifa
yanatumia kukabiliana na janga hili, lakini tatizo linaendelea kukua"
akasema Bw. Sam Kutessa wakati akifungua mkutano huo.
No comments:
Post a Comment