Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara.
Ni lugha
ya taifa kwa nchi za Kenya na Tanzania na pia yazungumzwa kwenye nchi za
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Visiwa vya
Comoro na nchi nyingine
Ikizungumzwa
na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio
lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa
Afrika.
Ni lugha
muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata
usalama miongoni mwa mataifa. Lakini , licha ya ukubwa wake, lugha hii
inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Hivi
karibuni, Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kilifanya
mkutano wake wa nne, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa pili wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Na amekuwa mkarimu sana
kujiunga nasi kuzungumzia juu ya lugha ya Kiswahili na changamoto zake
No comments:
Post a Comment