KLABU ya
Manchester United imepiga hatua katika harakati zake za kutaka kumsajili
Cesc Fabregas baada ya Mashetani hao Wekundu kuweka mezani Pauni
Milioni 26 kwa ajili ya kiungo huyo wa Barcelona.
Timu ya David
Moyes imekuwa ikihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Nahodha huyo wa
zamani wa Arsenal, ambaye amekuwa akipambana kuwa mchezaji muhimu kwa
mabingwa hao wa Hispania.
Lakini baada
ya kumkosa mchezaji mwenzake wa Barca, Thiago Alcantara kufuatia nyota
huyo wa timu ya taifa ya Hispania chini ya umri wa miaka 21 kuamua
kujiunga na Bayern Munich, tmabingwa hao wa Ligi Kuu England sasa wako
tayari kutumia fedha zaidi kuhakikisha mwanasoka huyo wa kimataifa wa
Hispania anarejea England.
Anarudi England? United imeipa Barcelona ofa ya Pauni Milioni 26 kwa ajili ya Fabregas
Klabu ya
zamani ya Fabregas, Arsenal inaweza kupiga bao katika dili ikitaka,
kutokana na The Gunners kupewa kipaumbele cha kumsajili mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 26.
Mtendaji Mkuu
wa United, Ed Woodward hivi karibuni amesema kwamba klabu iko tayari
kushindana kugombea wachezaji hata kwa dau la Pauni Milioni 60 hadi 70
na kwamba wanataka kusajili wachezaji wakubwa duniani.
Mtanashati: Fabregas akiwasili na mpenzi wake Daniella Semaan katika harusi ya mchezaji mwenzake wa Barcelona, Xavi Jumamosi
Ofa ya United
kwa Fabregas ni pungufu ya kiasi cha Pauni Milioni 5 kufika dau la
Pauni Milioni 30.75 ambalo linashikilia rekodi ya mchezaji wa bei mbaya
kusajiliwa na klabu hiyo, walipomnunua mshambuliaji wa Tottenham,
Dimitar Berbatov mwaka 2008.
Fabregas
alitimkia Barcelona akitokea Arsenal kwa Pauni Milioni 31 mwaka 2011,
lakini licha ya kuonyesha soka nzuri amekuwa akipambana ili kuwa
mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza akiwa na klabu hiyo ya La Liga.
Mashetani Wekundu? Fabregas (kushoto) na Robin van Persie wanaweza kuungana tena baada ya kuachana Arsenal
Ikiwa kiungo
huyo atakwenda Old Trafford, ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa
Arsenal, Robin van Persie, ambaye alicheza na Mholanzi huyo Kaskazini
mwa London kati ya mwaka 2004 na 2011.
Mspanyola
huyo ambaye alianzia soka ya ushindani kwa Washika Bunduki wa London na
kucheza jumla ya mechi 212 za Ligi Kuu, akifunga mabao 35 na kutoa pasi
za mabao 70 sasa ni mmoja wa wachezaji wakubwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment