Wakazi wa Wilaya ya
Ileje wanaoishi mikoa ya Iringa,Njombe,Rukwa na Mbeya Mjini,kwa pamoja
wamemuomba Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kuona umuhimu wa
kubadilisha mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya iliyopendekeza
makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe yawe eneo la Mkwajuni wilayani Chunya,kwa
madai kuwa ni mbali ukilinganisha na Jiografia ya wilaya ya ileje.
Wananchi wa wilaya
ya Ileje wametoa maombi yao wakati wa Kongamano lililoshirikisha wakazi wa
ileje wanaoishi Nje ya wilaya hiyo,lililofanyika katika ukumbi wa Kiwira Motel
Jijini Mbeya,wakijadiliana maendeleo ya wilaya hiyo pamoja na mgawanyo wa
mkoa wa Mbeya na kupata mkoa mwingine mpya,ambao wameomba mapendekezo ya makao
makuu ya mkoa huo yasogezwe.
Wakizungumza katika
Mkutano huo Wananchi hao wamedai kuwa umbali kutoka Wilayani Ileje kwenda Mbeya
Mjini ni mbali sana hivyo kuwapeleka Mkwajuni ni kuzidi kuwaongezea safari
zaidi.
Yohana Seme
Mkazi wa Ileje amesema lengo la kugawanya Mkoa ni kusogeza huduma kwa
Wananchi lakini Mapendekezo ya Kupeleka Makao makuu ya Mkoa Wilayani Chunya ni
kupokonya huduma kwa Wakazi wa Ileje ambao huduma nyingi hutegemea Nchi jirani
ya Malawi.
Mjadala wao
wanaileje ukaenda mbali zaidi,baada ya mapendekezo ya awali ya wajumbe wa
kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya,kupendekeza makao makuu ya mkoa wa Songwe
yawe ni Mkwajuni Kilometa 321 kutoka kusini mwa wilaya ya Ileje.
Kutokana na umuhimu
wa Kongamano hili,Mbunge wa Jimbo la Ileje Aliko Kibona ambaye pia
alikuwepo katika Mkutano huo alisema kwa niaba ya Wananchi wa Ileje hayuko
tayari kukubaliana na maamuzi ya Kupeleka Makao makuu Mkwajuni Wilayani Chunya.
Kibona amesema mapendekezo
ya Wanaileje ni kwamba Makao makuu ya Mkoa wa Songwe yasogezwe na kuwekwa
katika kijiji cha Henje wilayani Mbozi, mapendekezo ambayo yameungwa Mkono na
Wakazi wa Momba, Mbozi na Ileje yenyewe.
|
No comments:
Post a Comment