Waziri
Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akiwasili katika eneo la Bandari ya Dar es
Salaam tayari kwa kuzindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabomba
yatakayotumika katika ujenzi wa mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akishuhudia Balozi wa Jamhuri ya Watu wa
China Balozi Lu Youging alipokuwa akimalizia kufunua kitamba kama ishara
ya uzinduzi rasmi wa upakeaji wa mabomba ya Gesi
hdg
Na Frank Shija - Maelezo
Serikali imewatoa hofu wananchi wa Mtwara kuhusu kunufaika kwao na gesi asilia iliyopatikana katika maeneo yao.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo
Pinda alipokuwa akizindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabonba ya gezi
kwa ajili ya mradi wa bomba la kusafirishia Gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam mwisho ni wiki jijini Dare se Salaam.
Pinda
amesema kuwa wananchi wa watanzania watanufainaka na mradi huo hasa hasa
wakazi wa Mtwara kwakuwa vijana wengi watapata ajira wakati na baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo kwakuwa viwanda mbalimbali
vitajengwa mkoani Mtwara kikiwemo kiwanda cha Saruji ambacho ujenzi wake
umekwisha anza.
"Ndugu
zangu wana Mtwara ni waambe tu wakati wa kunufaina na rasilimali ya Gesi
sasa umefika,niseme tu mradi huu utakapokamilika fursa mbalimbali
zitafunguka ikiwemo ajira kwa wakazi wa Mtwara". Alisema Pinda.
Kwa
upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Balozi Lu
Youging amesema kuwa Tanzania itanufaika na mradi huu na kukua kiuchumi
kwakuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi katika nishati na badala
yake itazalisha nishati yakutosha.
Balozi
huyo aliongeza kuwa kutpitia mradi huu Tanzania itaondokana na kuwa
tegemezi katika shughuli zake za maendeleo kwa kuwa kuna hazina ya
kutosha ya gesi asilia na itawanufaisha watanzania wenyewe na si
vinginevyo.
Jumla ya
mabomba 3400 yamepokelewa katika awamu ya kwanza ambapo awamu ya pili
itapokelewa shehena yenye mabonmba 4600 katika bandari ya
Mtwara.Inakadiriwa kuwa jumla ya shehena 12 zitatumika mpaka mradi
utakapokuwa umekamilika.
No comments:
Post a Comment