Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano wa wandhi wa habari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)
Madereva wamepewa kipaumbele kwenye tume itakayokuwaikisimamia usafirishaji,kwani tume hiyo itakuwa na wajumbe watano kutoka Umoja wa madereva tuu na kutoka sekta nyingine watakuwa wajumbe watatu .
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Makonda amesema kuwa kamati hiyo haitaundwa na serikali, wajumbe watatokana na uchaguzi wa madereva wenyewe pia na wajumbe wengine watatoka Mamlaka ya usafirishaji (SUMATRA), TABOA , TATOA, Wizara ya Ajira, wizara ya na mambo ya ndani.
Makonda ameongezea kuwa Mgomo wa madereva hautakuwepo tena milele, madereva wachague wajumbe ambao wanaweza kuhakikisha haki zao kinasimamiwa vizuri na kutatua matatizo yao
No comments:
Post a Comment