Watoto wakipewa chanjo ya ugonjwa wa kupooza Polio nchini Pakistan
Wazazi wengi wanashuku kuwa chanjo hiyo ni sehemu ya njama ya mataifa ya Magharibi kupunguza idadi ya Waislamu
Mazishi ya mhudumu wa afya aliyeuawa na waislamu wenye siasa kali
Maafisa
wa utawala nchini Pakistan wametoa onyo kwa wazazi watakaokataa kuwapa
watoto wao chanjo ya kupooza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Maafisa
wa utawala katika jimbo kubwa zaidi nchini humo Baluchistan, wanasema
kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuenea upya kwa ugonjwa huo
hatari na hivyo kuwalazimu kuchukua tahadhari zaidi
Kulingana
na mpango huo mpya, kila mtoto atalazimika kuwa na cheti cha kuonesha
kuwa tayari amepokea chanjo hiyo ya kupooza kabla ya kupokea huduma
yeyote kutoka kwa serikali ikiwa ni pamoja na kuingia shuleni.
Familia
nyingi zinapinga watoto wao kupokea chanjo kufuatia uvumi kuwa ni njama
ya mataifa ya magharibi ya kuwahasi watoto wao kwa nia ya kupunguza
idadi ya waislamu duniani.
Makundi
ya kigaidi yamekuwa yakiwalenga maafisa wa afya wanaotoa chanjo hiyo
wakisema kuwa inawafanya watoto kushindwa kupata watoto wakitimiza umri
unaostahili.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment