Majaji
wapya wawili wa mahakama ya rufaa Augustine Mwarija na Stella-Esther
Mugasha wamesema changamoto inayowakabili ni ya kuhakikisha haki
inatendeka na kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuondoa msongamano wa
mashauri.
Majaji hao wameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya
kuapishwa na rais Jakaya Kikwete kuwa majaji wa mahakama ya rufaa
wakitokea mahakama kuu ambapo Mwarija, alikuwa jaji mfawidhi, mahakama
kuu, divisheni ya biashara huku Mugasha akiwa jaji mfawidhi mahakama kuu
kanda ya Dar es Salaam.
Wakizungumza katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu majaji hao
wameahidi kutumia uzoefu walionao katika kukabiliana na changamoto ya
wingi wa mashauri katika mahakama hiyo kwa kutumia utaratibu wa
kushughulikia kwanza mashauri ya yaliyochukuwa muda mrefu kutolewa
maamuzi.
No comments:
Post a Comment