Thursday 25 June 2015

Serikali yatakiwa kutoa kodi kwenye vyanzo vikubwa.



Baadhi ya wabunge wameitaka serikali kupambana na vyanzo vikubwa vya uhakika vya kodi ikiwemo makampuni ya simu za mkononi badala ya kuongeza kodi kwenye mafuta na kusababisha wananchi kuishi katika mazingira magumu.

Wakichangia mswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2015, baadhi ya wabunge wamehoji uwezo wa serikali wa kuyakabili makampuni makubwa ili yaweze kulipa kodi hususani katika mfumo wa soko huria ambapo baadhi ya makampni yamekuwa na mapato makubwa kuliko ya serikali.

 
Awali akiwasilisha maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti, Mheshimiwa Josephat Kandege amesema kutokana na kutokuwa na tafsiri sahihi ya mafuta ghafi serikali imekuwa ikikosa mapato stahiki na kuitaka kufanya uchunguzi, huku msemaji wa kambi ya upinzani Mhe.Joseph Mbatia akiendelea kusisitiza kuwa kuongeza kodi katika mafuta kutawaumiza wananchi.
 
Aidha akiwasilisha mswada wa sheria ya fedha hususani matumizi ya sukari inayotumika viwandani, waziri wa fedha na uchumi Mhe Saada Mkuya Salum amesema serikal imepunguza kodi hadi asilimia 25 kutoka asilimia 50 ya awali kwa waagizaji wa sukari ili kutoathiri mitaji ya wafanyabiashara.

No comments: