.
Chama
cha demokrasia na maendeleo chadema kimeitaka serikali pamoja na tume
ya taifa ya uchaguzi,ipate fundisho kufuatia zoezi linaloendelea hivi
sasa nchini la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ambapo
wananchi wanajisimamia wenyewe bila ya kuwepo kwa askari polisi vituoni,
na zoezi linaendelea kwa utulivu na amani, hali inayoashiria kuwa
askari hao ndio wanakuwa chanzo cha uvunjifu wa amani wakati wa zoezi la
kupiga kura vituoni.
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA
Dakta.Wilbroad Slaa,akiongea na wakazi wa mji wa Namanyere wilayani
Nkasi mkoani Rukwa,amesema haoni kwanini kunakuwa na lundo la askari
polisi kwenye vituo vya kupigia kura ambalo ni zoezi la kidemokrasia,
hali ambayo mara nyingi inaishia kusababisha vurugu na kuwaacha watu
wengi wakipoteza maisha na wengine kuwa walemavu, kama katika chaguzi
nyingi zilizopita ikiwa ni pamoja na ule wa serikali za mitaa mwishoni
mwa mwaka jana.
Aidha katibu mkuu huyo amewataka wananchi waendelee kujitokeza kwa
wingi kujiandikisha kwenye daftari hilo,ili waweze kuitumia haki yao ya
kimsingi ya kupiga kura, na kwamba wasitegemee hata siku moja kama tume
hiyo itawafuata majumbani mwao kuwalazimisha kwenda kujiandikisha.
No comments:
Post a Comment