Wednesday, 3 June 2015

Watendaji wa mkoa wa Kilimanjaro watakiwa kusimamia daftari la wapiga kura kwa umakini.


Watendaji wa wilaya mkoani Kilimanjaro wametakiwa kusimamia vema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la kupiga kura katika kuhakikisha wanaoandiskishwa ni raia wa Tanzania kutokana na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Siha kuwa na idadi kubwa ya wananchi ambao sio  watanzania.

Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Bw.Leonidas Gama ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa halimashauri wa wilaya mkjoani kilimanjaro juu ya matumizi ya mashine za BVR ambazo zimewasili mkoani kilimanjaro kwa ajili ya zoezi la uandikishaji wa daftari la kupiga kura.
 
Amesema ni vema watendaji wote wakawa makini katika zoezi hilo la uandikishwaji pamoja na wanasiasa kuweka wawakilishi katika vituo vitakavyotumika kuandikisha ili kuepuka malumbano yasiyo ya lazima.
 
Kwa upande wake afisa uandikishaji tume ya uchaguzi Bi.Zena Chelamila amesema zoezi la kuandikisha litadumu kwa mwezi mmoja na kwamba vifaa vilivyowasili mkoani Kilimanjaro vinatosha kuandikisha wananchi wote.
 
Naye mweneykiti wa tume ya uandikishaji mkoa wa kilimanjaro bw.rashidi kitambulio na mkurugenzi wa manispaa ya moshi shaban ntarambe  wamesema wamejipanga kufanikisha zoezi hilo kwa ufasaha na kwamba wilaya ya siha ina watu zaidi 147 ambao sio raia wa Tanzania.
 

No comments: