"Namshukuru
mke wangu kwa kunitia moyo kwakuwa alisikia na kuambiwa mengi tangu mwanzo wa
sakata hili....kuwa mumewe(Silla Yalonde) ni mshenzi..mwizi..mnafiki ....mnazi
wa kutupwa wa Yanga,mtu mwenye tamaa na fedha nk nk...lakini aliyavumilia na
kunitia moyo kwakuwa anajua weledi wangu tangu tukisoma pamoja pale Vwawa Day
miaka ya 98 hadi kesho..asante nyingi kwake..
Thanks
friends kwa kunitia moyo...kunipa ushauri muda wote....
Kwa
ufupi niwashukuru Yanga kwa kitendo cha kiungwana kwanza kwa kutuandikia barua
ya kutuomba radhi kwa maneno na lugha chafu yaliyotolewa na msemaji wao dhidi
ya mkurugenzi wa klabu yetu na klabu yetu kwa ujumla...
Zaidi
niseme tu Dr Tiboroha ni kiongozi wa aina ya kipekee...anajua
anachokifanya...achilia mapungufu madogomadogo ya kibinadamu na kimfumo ya
klabu yake lakini naiona Yanga imepata mtu sahihi na in the near future
atawapelekea mahali fulani pazuri...nakiri wazi kuwa huyu ndiye role model
wangu nina mengi ya kujifunza kutoka kwake..na bahatimbaya hii imekuwa yenye
manufaa makubwa sana kwa klabu ya Kimondo lakini mimi binafsi haswa ktk career
development yangu.
Yanga
wametimiza masharti yote ya kumsajili Mwashiuya na kuanzia hivyo ni mchezaji
wao halali...
Wametupatia
pesa taslimu na zaidi kufikia makubaliano yaliyo katika maandishi na kusainiwa
na mimi na Katibu wa Yanga Dr Tibo kuwa itapigwa game ya kirafiki hapa kwetu
Mbozi na mapato yote yatachukuliwa na klabu yangu pendwa...hili litaimarisha
mahusiano baina yetu na klabu ya Yanga...ni hatua kubwa saana kwa soka letu.
Tumewaandikia
barua Tff kuhusiana na issue ya Jerry hope mtalisikia suala lake huko na sio
kwetu tena...
Nimalizie
kwa kusema weledi wetu ktk utendaji wa shughuli zetu za kila siku una tija mara
nyingi zaidi kuliko blabla tunazozikumbatia...
"Lets
act professional in issues.."Mabadiliko ya kweli yanaanza na wewe...
Asanteni"
Silla
Yalonde, Katibu Mkuu Kimondo
No comments:
Post a Comment