Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Rished Bade akiwaeleza
wajumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi kuhusu kuanza kutumika
kwa sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 2014 iliyoanza
kutumika kuanzia Julai 1, 2015 na jinsi itakavyobadilisha baadhi ya
mifumo ya kibiashara,wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya
Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Jijini
Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia akimshukuru
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa
kuhudhuria ufunguzi wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) na kuahidi kuwa
washiriki wazuri katika mabadiliko katika sekta ya Kodi nchini,wakati
wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa
ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na
Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akimueleza
jambo Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi na mwenyekiti wa
Kamati ya sekta ya Umma Bw.Nicholus Duhia, katikati ni Bi. Diana Masalla
Meneja Elimu kwa Mlipakodi.
Yona
Kilagane akiwasilisha mada wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka
ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA)
Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Rished Bade akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.
Na Hassan Silayo, MAELEZO
Mamlaka
ya mapato Tanzania (TRA) imedhamiria kufikia malengo yake katika
ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kufikia shilingi trilioni
22.3 iliyojiwekea katika bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016.
Hayo
yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania Bw. Rished Bade wakati wa Semina ya wahasibu iliyoandaliwa na
Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi
(NBAA) ikiwa na lengo la kujadili kuhusu masuala ya kodi, bajeti na
uchumi kwa ujumla.
“Moja
kati ya malengo tuliyojiwekea sisi kama mamlaka ni kuisaidia serikali
katika ukusanyaji wa mapato tukiwa na lengo la kuiwezesha kufikia kiasi
cha shilingi trilioni 22.3 zilizopangwa kutumika katika mwaka huu wa
fedha” Alisema Bw.Rished.
Akieleza
kuhusu sheria mpya ya kodi iliyoanza kutumika julai 1, 2015 Bw. Rished
alisema kuwa kuwa sheria hii inategemewa kubadilisha baadhi ya mifumo ya
kibiashara nchini.
Pia
alieleza kuwa kitu muhimu kwa sasa ni wajumbe wa bodi hiyo kukaa na
kuipitia sheria hiyo na kuangalia mabadiliko yaliyomo na wao kama wadau
katika sekta hiyo kusaidia katika kuboresha mazingira ya kibiashara.
Naye
Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia
alimshukuru Kamishna Mkuu kuhudhuria semina hiyo na kuahidi kuwa
washiriki wazuri katika mabadiliko ya sekta ya Kodi nchini
“Ndugu
Kamishna Mkuu, umekuwa ukishirikiana na kufanya kazi kwa karibu na bodi
hii, hivyo tunakuahidi baada ya kumaliza semina hii tutakuwa washiriki
wazuri hasa katika mabadiliko ya sekta ya Kodi nchini” Alisema Bw.
Duhia.
Aidha,
Mshiriki wa Mafunzo hayo na muwakilishi kutoka Jubilee Insurance Bi.
Hellena Mzena alisema kuwa kikubwa anachotegemea kujifunza kutoka kwenye
semina hiyo ni jinsi gani sekta ya Bima ilivyoguswa kwa mara ya kwanza
katika Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 na jinsi
gani wataenda sambamba na mabadiliko hayo
No comments:
Post a Comment