JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 09.07.2015.
·
MTU MMOJA AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA
MWILI WAKE KUTUPWA.
·
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI.
·
WATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAVAMIA NA
KUJERUHI MAPADRI 3 NA MAPADRI WANAFUNZI 03 NA KISHA KUPORA MALI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA MKAZI WA KAFUNDO – IPINDA AKIWA NA BHANG
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI
WA IDENDELUKA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MICHAEL JAILOS (29) ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA RUNGU KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA
MWILI WAKE KUTUPWA JIRANI NA SHULE YA MSINGI IDENDELUKA.
MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA JIRANI NA SHULE HIYO MNAMO TAREHE 08.07.2015 MAJIRA YA SAA
09:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA IDENDELUKA, KIJIJI/KATA YA SANGAMBI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA CHANZO
CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI. UPELELEZI UNAENDELEA ILI KUWABAINI/KUWAKAMATA
WAHUSIKA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KWENYE TUKIO HILO AZITOE KWENYE MAMLAKA
HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA
MIGUU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA TATU
WILSON (30) MKAZI WA IMEZU
AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA
MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 08.07.2015
MAJIRA YA SAA 20:07 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA DARAJANI-IMEZU, KATA YA INYALA, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. DEREVA
ALIKIMBIA NA GARI BAADA YA TUKIO. UPELELEZI NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA DEREVA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEHUSIKA KWENYE TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA SHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
WATU
WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAVAMIA NA KUJERUHI NA KISHA KUPORA MALI
MBALIMBALI BAADA YA KUWEKA KIZUIZI CHA MAWE/MAGOGO KATIKA BARABARA YA
MBALIZI/MKWAJUNI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA
SAA 02:00 HUKO ENEO LA MSITU WA MLIMA MSANGAMWELU, KIJIJI CHA MJELE, KATA
YA MSHEWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA BAADA YA
WATU WASIOFAHAMIKA WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI KULIWEKEA VIZUIZI GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI SM 3496 AINA YA
TOYOTA LAND CRUISER MALI YA HOSPITALI YA MWAMBANI CHUNYA LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA LOVED MWANDONGO
(53) MKAZI WA MKWAJUNI.
GARI HIYO
ILIKUWA IMEBEBA MAPADRI WATATU NA MAPADRI WATATU WANAFUNZI AMBAO NI 1. FURAHA HENJEWELE (36) PADRI MWANAFUNZI, MKAZI WA MBEYA
ALIPIGWA FIMBO KICHWANI NA KUKATWA PANGA MKONO WA KULIA 2. PADRI GASPER MWASHIMWANGA (37)
MKAZI WA MPUGUSO – TUKUYU ALIPIGWA FIMBO MWILINI 3. HENRY MWALYANGA (33) PADRI
MWANAFUNZI, MKAZI WA MBEYA ALIPIGWA FIMBO MWILINI 4. ELIAKIM KASEGILA (27)
PADRI MWANAFUNZI, MKAZI WA PERAMIHO ALIJERUHIWA MWILINI 5. PADRI BONIFASI CHALO (46)
MKAZI WA MWANJELWA ALIJERUHIWA KWA FIMBO MWILINI 6. EXAVERY MWAFUMBO (28)
PADRI MWANAFUNZI, MKAZI WA MWANJELWA NA 7.
DEREVA MWENYEWE LOVED MWANDONGO (53) ALIPIGWA FIMBO MWILINI.
AIDHA KATIKA
TUKIO HILO WAHANGA HAO AMBAO WALIKUWA WANAKWENDA GALULA KUHUDHURIA SHEREHE YA
UPADRISHO, WALIPORWA PESA TASLIMU AMBAZO BADO KUFAHAMIKA KIASI GANI, MABEGI YA
NGUO MBALIMBALI, ZAWADI ZA WAUMINI, SIMU
ZA MIKONONI PAMOJA NA MAJOHO. WAHANGA
WAMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.
MSAKO MKALI
UNAENDELEA ILI KUWABAINI WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ILI WAKAMATWE NA HATUA
ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KAFUNDO-IPINDA WILAYANI KYELA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GABRIEL
MWAKALEBELA (26) AKIWA NA BHANGI
UZITO WA GRAM 250.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 08.07.2015
MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO IPINDA,
KATA YA IPINDA, TARAFA YA NTEBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment