Pamoja
na mvutano mkubwa ulioibuka kutoka kwa vyama vya siasa na tume ya
uchaguzi ya Zanzibar hatimaye vyama hivyo vya siasa vimesaini
makubaliano ya maadili ya uchaguzi mkuu.
Mvutano huo uliibuka baada ya viongzoi wa vyama hivyo vya siasa
kukataa kusiani makubaliano hayo kwa madai ya kutokuwepo kwa wawakilishi
wa CCM na jeshi la polisi hali iliyosababisha mabishano na kutaka kikao
hicho kiahirishwe hadi CCM na polisi wawepo katika zoezi la uwekaji
saini.
Hata hivyo baada ya mwakilishi wa CCM kutokozea na bado zoezi hilo
lilikuwa gumu mbapo ukosefu wa polisi ndio sababu nyengine lakini baada
ya mabishano makali huku vyama vyingine kutishia kuondoka, wawakilishi
hao wa vyama walikubali kusaini baada ya busara za mwenyekiti wa kamati
ya maadili Bw Nassor Khamis huku kamati hiyo ikiahidi kuhakiksha jeshi
hilo linaweka saini hiyo baadae.
Akizungumza baada ya kumalizika zoezi hilo mwenyekiti wa tume ya
uchaguzi Bw Jecha Simai Jecha aliwahakikshia viongzoi wa vyama hivyo ZEC
itatekeleza wajibu wake na uadilifu mkubwa huku mwaklishi wa UNDP ambao
ndio wafadhili wakubwa wa ZEC kuwataka viongozi wa vyama hivyo
kuyaheshimu maadili na makubaliano hayo.
Baadhi ya makubaliano yaliyosainwa na vyama hivyo 22 vya siasa ni
kuhakisha kampeni za ustarabu, kuepukana na matusi na kuheshimiana na
kufuatwa kwa sheria za nchi.
No comments:
Post a Comment