Monday, 23 January 2017

MBEYA WALICHANGAMKIA SHINDANO LA SHINDA NYUMBA


Na Derick Lwasye, Mbeya 
SHINDANO la shinda nyumba na Global Publisher awamu ya pili limepokelewa kwa vizuri na wasomaji wa Magazeti ya Global Publisher Kampuni namba moja ya uchapishaji wa Magazeti Tanzania.

Hii ni mara ya pili kwa Shindano hili la shinda nyumba kufanyanyika, huku awamu ya kwanza akipatikana mshindi wa mjengo wenye thamani ya mamilioni kutoka mkoani Iringa, Nelly Mwangosi.

Wakizungumza na Championi wakati wa promosheni ya Shindano hilo lililofanyika kwenye maeneo Mbalimbali ya viunga vya jiji la Mbeya, wasomaji hao walisema wana uhakika na kile kinachofanywa na Global Publisher tofauti na makampuni mengine ambayo yanaonekana kumwandaa mshindi.

"Siyo siri ninyi jamaa Mkoa vizuri sana na hamna magumashi kwenye bahati Nasibu zenu, hivyo nimejipanga kununua kopi nyingi za magazeti ya Global Publisher ili nijitengenezee mazingira mazuri ya kuibuka mshindi "alisema Mussa Hassan ambaye ni Dereva Bajaji kwenye Kituo cha Kabwe.

Rodrick Robin maarufu kama mzee wa ijumaa wikienda, alisema huu ndiyo wakati wa kujaribu bahati yake kutokana na kuwa mteja mzuri wa Gazeti la Ijumaa ambalo huwa limesheheni Hadithi zenye msisimko.

"Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa wa Magazeti ya ya Global Publisher ila nilikuwa sitilii maanani Mashindano yaliyokuwa yakiendeshwa kutokana na kutoamini kama mshindi anapatikana bila kupangwa, ila baada ya kuona mshindi wa awamu ya kwanza kapatikana kutoka Iringa tena ni mwanamke mjasiliamali nikashawishika sana, na sasa tutakula sahani moja mpaka kieleweke "alisema

Katika eneo la Nanenane ambapo ndiyo kuna stand ya mabisa ya wilayani na mikoani, wasomaji wa magazeti ya Global Publisher walionekana kufurahia awamu hii ya pili ya shinda Nyumba na Global Publisher.

Kwa upande wao wauza magazeti wa jiji la Mbeya na nyanda za juu kwa ujumla wamewataka Mawakala wa magazeti ya Global Publisher kuagiza Nakala nyingi ili kuepusha usumbufu kama ulivyojitokeza awamu ya kwanza ya Shindano hili.

"Unajua Shindano hili ni Shindano kubwa sana hapa Tanzania, hivyo kila mtu atataka kujaribu bahati yake, tunawaomba mawakala wajitahidi kuagiza nakala za kutosha ili kuwaondolea usumbufu wasomaji na wateja wetu, msimu uliyopita kulikuwa na uhaba wa nakala, hivyo kuna baadhi ya wasomaji walikuwa wanakosa nakala.

Maeneo mengine ambayo promosheni hiyo ilifanyika ni Mbalizi, Uyole, Mwanjelwa, Soweto, Iyunga na Sokomatola. 

No comments: