Monday 23 January 2017

MABONDIA NANE KUZICHAPA MATEMA BEACH SIKU YA IJUMAA 

Na Derick Lwasye, Mbeya Mpambano mkali wa masumbwi usiyokuwa wa ubingwa unatarajia kufanyika ijumaa ya wiki hii katika ukumbi wa Matema Beach wilayani kyela.

Mpambano huo unahusisha mabondia nane kutoka wilaya za Kyela, Rungwe na Mbeya mjini kwenye uzito wa middle weight.

Katika pambano la kwanza, Bondia Maisha samson maarufu kama Kyela one kutoka kyela atapambana na Alex Mwakibete toka wilaya ya Rungwe, Mchezo huo utakuwa wa raundi kumi.

Mapambano mengine yatakuwa kati ya Bondia Six Mashine na Boniphace toka mbeya,Moses Mwamlanda atazichapa na mwakabyabya(mataslim)wote kutoka wilayani kyela, mapambano yatakuwa ya raundi nane. Mpambano wa mwisho ni kati ya Joshua Milton  dhidi Shaban Mwampela nao utakuwa wa raundi nane.

Akizungumza na Championi mratibu wa mapambano hayo James Mwakyembe, alisema maandalizi yamekamilika na mapambano hayo yamedhaminiwa na Kituo cha Radio cha Kyela FM.

"Maandalizi yamekamilika na siku ya alhamisi itakuwa siku ya kupima uzito kabla ya kupanda ulingoni siku inayofuata ya ijumaa. Lengo hasa la kuandaa mapambano haya ni kutaka kuinua mchezo huu wa ngumi ambao ulianza kupotea hapa wilayani Kyela "alisema Mwakyembe.

No comments: