Mbunge
wa Mtama, Mh Nape Nnauye amefunguka na kusema hatua mbalimbali
zilizochukulia na serikali ikiwepo kubana matumizi, kufukuza wafanyakazi
hewa, kuongezeka kwa mapato kama hazita tafsiriliwa kwa maboresho ya
huduma za jamii ni sawa na kazi bure.
Nape
Nnauye alisema hayo jana wakati akichangia katika bajeti ya Wizara ya
Maji na kusema serikali inapaswa kufanya mambo kwa kuwafurahisha
wananchi kwa kuwapa huduma bora na si vinginevyo.
"Serikali
ya awamu ya tano ilipoingia madarakani ilianzakuchukua hatua kadhaa za
kuongeza mapato ya serikali, ikiwa ni pamoja na kubana mianya ya wakwepa
kodi lakini kupunguza matumizi ikiwemo kupunguza safari, kupunguza
sherehe na matumizi ambayo kiukweli kwa namna nyingine yalionekana si ya
lazima, ikiwemo kushughulika na wafanyakazi hewa.
"Lakini
pia kwa takwimu tunaambiwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7.2 haya yote
hayatakuwa na maana kama hayata tafsiriliwa kwenye maboresho ya huduma
za jamii na hasa maji.
"Hatua
hizi lengo lake lilikuwa kuongeza uwezo wa serikali sasa kama hatua
hizi zimechukuliwa na matokeo yake ni chanya tunapaswa tuyaone kwenye
ongezeko la huduma za jamii, tusipofanya hivi hatua tulizochukua
zitakuwa hazina maana hata kidogo, bajeti iliyopita tulitenga bilioni
mia tisa bajeti hii tukiwa tumesimamimia hatua tulizochukua ambazo
kiukweli zingeongeza uwezo wa Serikali tunatoka mia tisa na kwenda mia
sita, kwa vyovyote vile Watanzania hawawezi kutuelewa" alisema Nape Nnauye
Nape
Nnauye aliendelea kusisitiza kuwa wananchi hawawezi kuielewa serikali
kama hatua inazochukua haziendi kubadilisha maisha yao ya kila siku,
lakini Mbunge huyo alisema tatizo la maji lipo katika kila jimbo nchi
hii sema kinachotokea wanapishana ukubwa wa tatizo.
"Ilani
hii ya Chama Cha Mapinduzi ndiyo mkataba wetu kati ya CCM na wananchi
tusipoitekeleza wananchi hawatoturudisha na huu ndiyo ukweli kwa sababu
tuliwaahidi Mh Naibu Spika na bahati mbaya tatizo la maji pamoja na
kuwaathiri watu wote lakini wakina mama ambao ndiyo wapiga kura wakubwa
wa CCM ndiyo waathirika wakubwa wa tatizo hili ndiyo maana sina mashaka
kwamba serikali itasikiliza na kwenda kuongeza pesa" alisema Nape Nnauye
No comments:
Post a Comment