Kitendo cha kujeruhiwa kwa risasi mbunge wa singida mashariki tundu lissu (Chadema) alhamis kimemuibua katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF) maalim seif sharif hamad akilitaka Jeshi la polisi kuhakikisha linawatambua na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa tukio hilo.
Maali m Seif ameeleza kuwa kuendelea kwa vitendo hivyo bila kuchukuliwa hatua ni sawa na kutoa Baraka vitendo hivyo viendelee jambo ambalo alisema linatia hofu na kutishia uchumi wa nchi.
Alifungua mkutano mkuu wa viwanja wa CUF wilaya ya kaskazini A unguja
alisema matukio ya vitendo vya uvunjifu wa amani yamekuwa mengi hivyo
bila kuchukuliwa hatua vitaleta athari kubwa kwa taifa.
“Jeshi la polisi linataka kudumisha amani kwa raia ni vyema likahakikisha wahalifu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria”
“kitendo alichofanyiwa Lissu ni cha kinyama na kikatili ambacho hakivumuliki katika ulimwengu huu na wahusika wa tukio hilo walipaswa kuwa wameshakamatwa.

No comments:
Post a Comment