Tajiri
namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa
hapa nchini amemtahadhariha Rais John Pombe Magufuli kuwa sera zake
mpya zinawaogopesha wawekezaji.
Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani milioni 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema ni wakati umefika kwa raisi Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini .
Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani milioni 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema ni wakati umefika kwa raisi Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini .
Dangote
ameyasema hayo katika mkutano wa FT Afrika unaofanyika London Uingereza
na kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Mwekezaji
huyo ameeleza kuwa Uhusiano wake na Rais Magufuli ni mzuri lakini
akashauri Rais azipitie upya sera zake kama anataka kuwavutia
waekezaji wengi zaidi.
“Uhusiano
wangu na Rais Magufuli uko sawa lakini Tanzania lazima itazame upya
sera zake kama inataka kuvutia wawekezaji,” alisema Dangote.
Dangote
pamoja na watu wengine mashuhuri wakiwemo viongozi wa maeneo mbalimbali
duniani wamehudhuria mkutano huo wa FT Africa wenye lengo la kuangazia
changamoto zinazolikumba bara la Afrika na namna ya kuzitatua
unaofanyika kila mwaka na mwaka huu umefanyika huko London, Uingereza
kuanzia Oktoba 8 hadi Oktoba 9.
Kauli
mbiu ya mkutano huo ni ‘what is working in Africa’ ikiwa na maana ya
‘nini kinachofanya kazi katika Afrika’ ikiwa na dhumuni la kuangazia ni
kwa namna gani bara hilo linaweza kunufaika kutokana na fursa,
rasilimali na utajiri uliopo humo.
No comments:
Post a Comment