Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amefunguka na kusema
kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na
mwanadada Mange Kimambi na kusema kuwa jeshi la polisi linashughulikia
suala hilo.
IGP
Sirro amesema hayo jana alipokuwa mjini Iringa kwenye ziara ambapo
alisema kuwa jeshi la polisi linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya
kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ambaye amekuwa
mkosoaji wa mambo mbalimbali na kutoa machapisho ambayo serikali inaona
ni ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake.
Aidha
IGP Sirro alisema kuwa kwa sasa hawawezi kuweka wazi ni hatua gani
zinachukuliwa dhidi ya mwanadada huyo ambaye kwa sasa anaishi nchini
Marekani
Mbali
na hilo IGP Sirro alisema jeshi hilo halitawavumilia maafisa wa polisi
na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto kwa
kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa sheria
huku akiwataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika kushughulikia
makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa na viongozi
wengine.
No comments:
Post a Comment