Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameiagiza Mamlaka
ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi
zao ili kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima.
Akiongea
katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka
ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA) leo na kuwahusisha Watumishi wote wa
Taasisi hiyo, Dkt. Mwanjelo amewataka watumishi hao kuwa na malengo na
mpango kazi ambao kila mtu atautekeleza na atapimwa kutokana na mpango
kazi huo.
Hata
hivyo Dkt. Mwanjelo amewapongeza kwa namna wanavyotekeleza majukumu
yao kwa sasa, hususan katika zoezi la uagizaji wa mbolea kwa mfumo wa
pamoja (Bulk Procurement System) ambao umechangia kwa kiasi kikubwa
mbolea hiyo kumfikia mkulima kwa bei nafuu.
Pamoja
na pongezi hizo Naibu Waziri, Dkt. Mwanjelwa ameitaka TFRA kuongeza
bidii katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha kuwa wanaondoa kero
zinazowakabili Wakulima.
Aidha
ameitaka Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea kuhakikisha kuwa mambo matatu
muhimu yanazingatiwa ambayo ni upatikanaji wa mbolea (Availability)
ufikishaji wa mbolea karibu zaidi kwa Wakulima (Accessibility) na kwa
bei ambayo wakulima wanaweza kumudu kuinunua (Affordability)
“Mhakikishe
mbolea inakuwepo nchini kote na wakulima wanapohitaji inapatikana na
iwe kwa gharama ambayo Mkulima anaweza akanunua. “Amekaririwa, Naibu
Waziri.
Naye
Kaimu Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo bwana Lazaro Kitandu amemshukuru
Naibu waziri kwa kuwatembelea na kuwatia moyo katika utendaji kazi wao
na kumhakikishia kwamba TFRA imejipanga vizuri kupambana na changamoto
za baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hasa katika kuzingatia
bei elekezi ya mbolea.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza
viongozi pamoja na wafanyakazi katika kikao kazi kilichofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA)
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akipata maelezo
kuhusu sampuli ya mbolea aina ya DAP kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa
Mamlaka ya Mbolea (TFRA) Bwana Lazaro Kitandu alipotembelea ofisi hiyo.
No comments:
Post a Comment