Friday 9 March 2018

MWASELELA FOUNDATION YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI DARAJA LA NNE


Na Derick Lwasye ,Mbeya

Wakati ligi daraja la nne ngazi ya wilaya ya Mbeya jiji  ikiwa imefika tamati hivi karibuni na Ikuti fc kufanikiwa kujinyakulia ubingwa huku Isanga Rangers wakishika nafasi ya pili .

Mdhamini wa ligi hiyo Mwaselela Foundation amekabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo iliyoshirikisha timu 15 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Mbeya.

Zawadi zilizotolewa ni shilingi milion moja (1,000,000) kwa mshindi wa kwanza ambaye ni Ikuti fc ,wakati Isanga rangers wao walikabidhiwa kitita cha shilingi laki tano (500,000) ambayo ni zawadi ya mshindi wa pili.

Zawadi zingine zilizotolewa ni Shilingi laki tatu (300,000) ambazo zilinyakuliwa na Morning star ambayo imekuwa timu yenye nidhamu kwenye ligi hiyo,zawadi ya mfungaji bora ilinyakuliwa na Reston Richard ambaye alikuwa na mabao 12 aipewa kiasi cha shilingi laki moja,naye golikipa bora Ravagan Salangeli naye alijipatia kiasi cha shilingi laki moja.

Chama cha soka wilaya ya Mbeya jiji (MUFA) kilitoa vyeti kwa mdhamini wa ligi hiyo,Ndele Mwaselela pamoja na vilabu vyote vilivyoshiriki ligi hiyo.


No comments: