MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2012 YATANGAZWA
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa leo ametangaza matokeo ya Mtihani wa
Darasa la Saba 2012 uliofanyika nchini kote tarehe 19 na 20 Septemba,
2012.
Katika Mtihani huo Jumla ya
wanafunzi 894,881 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambapo wavulana ni
426,285 sawa na asilimia 47.64 na wasichana ni 468,596 sawa na
asilimia 52.36. Aidha, kati ya wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379
ambao walitarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na
wanafunzi 20,502 walitarajiwa kufanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo
ndiyo waliyoitumia kujifunzia.
Wanafunzi wasioona waliosajiliwa
kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na
wasichana 39. Watahiniwa
wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao
wavulana ni 238 na wasichana ni 257.
No comments:
Post a Comment