Mbunge wa viti maalum (CCM) Ritta Kabati akiingiza mashairi katika wimbo mpya akishirikiana na vijana chupikizi 20 wa kabati star search katika studio za Top Magic Sound zilizoko Ipogoro Iringa mjini.
Muziki wa kizazi kipya wengi wanaujua kama bongo fleva wazidi kuwavutia viongozi mbalimbali na wengine wanaimba hadi sasa kama Joseph Mbilinyi aka Sugu, Vick Kamata sasa amejitokeza mbunge mwengine wa viti maalum toka chama cha mapinduzi Ritta Kabati na kuufanya uwe gumzo katika maisha ya watanzania na nchi za jirani kitu kinachofanya watu mbalimbali kujitokeza kuupenda na wengine kuamua kuingia kwa kasi katika tasnia hii ya burudani Tanzania.
Katika kuukuza zaidi muziki huu Mbunge wa Viti maalum kupita chama cha Mapinduzi mkoani Iringa Ritta Kabati akishirikiana na wasanii chipukizi 20 wa kwanza waliotokana na shindano la kutafuta vipaji la Kabati Katiba Star Search amefanikiwa kutoka wimbo mmoja unaokwenda kwa jina la 'Iringa Bila Ukimwi Inawezakana' uliofanywa katika studio za Top Magic Sound chini ya mzalishaji anayekuja kwa kasi pande za Nyanda za juu Kusini Ecko Msigwa.
Wimbo huo ni harakati za mbunge Kabati alizozianzisha katika kuwakomboa vijana katika majanga kama uvutaji wa bangi, kuepukana na maambukizi ya ukimwi katika mkoa huu ambao unaongoza kwa sasa nchini Tanzania na amesema kwamba wakati anafikiria kuingiza mashairi hayo kwa kweli alikuwa katika hali ya huzini kwa jinsi vijana walivyoweza kufanya vizuri katika wimbo huo kwa lengo la kuwakomboa watanzania kupitia muziki.
Baadhi ya mashairi ya hayo ni ‘ndugu zangu watanzania nina maumivu makali sana, tumepoteza ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu dira ya maendeleo inateketea ni wakati wetu kupambana iringa bila ukimwi inawezekana’ “ kwa kweli nina uhakika wa kuwafunika vijana hawa katika wimbo huu ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa mkoa huu kwa kuwa ni mkusanyiko wa vipaji vya kweli vilivyotokana na shindano nililoandaa” alisema Kabati
Wimbo huo unatarajia kuzinduliwa rasmi leo katika radio zote za Nyanda za Juu Kusini na kisha kusambazwa katika radio zote nchini Tanzania na amewataka wadau kuwapa nguvu vipaji hivi kwa kununua kazi za vijana kwa lengo la kuwaongeza kipato na kuondoka na maisha ya vijiweni.
No comments:
Post a Comment