Ahadi Mwandeko (22) amenyofolewa nyama mkononi
akiwa usingizini.
|
MWALIMU wa Shule ya msingi Motomoto iliyoko
katika kijiji cha Motomoto kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali Mkoani hapa, Ahadi
Mwandeko (22) amenyofolewa nyama mkononi akiwa usingizini.
Mwalimu huyo ambaye alikutwa na jeraha katika
mkono wake wa kulia asubuhi baada ya kutoka kuamka alisema hajia ni kitu gani
kilichomzuru hadi kufikia kuwa na jeraha kubwa mkononi.
Akizungumzia mkasa huo alipotembelewa na
waandishi wa habari shuleni kwake Mwalimu Mwandeko alisema akiwa usingizini
aliota kama anaugomvi na mwanamke ambaye hakuitambua sura yake, lakini baada ya
kuamka asubuhi alijikuta akiwa na jeraha huku likivuja damu nyingi.
Alisema baada ya kukuta hali hiyo alienda kwa
Mwalimu mkuuwa shule hiyo Lyidia Mdowe kwa ajili ya kumpa taarifa ya jambo
lililomkuta ambapo alishauriwa kwenda Hospitali kwa ajili ya matibabu.
Aliongeza kuwa baada ya kufika katika Zahanati ya
Ruiwa alipatiwa matibabu na kurejea shuleni ambapo Mwalimu mkuu alitoa taarifa
kwenye Serikali ya kijiji ambapo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Kassim Mwagalla
aliitisha mkutano wa hadhara.
Mwalimu Mkuu Mdowe alisema hali hiyo imezua
hofu kwa walimu wengine ambao ni wageni kiasi kwamba hata ari ya ufundishaji
imepungua baada ya kuona yaliyotendeka kwa mwalimu mwenzao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho
Kassimu Mwagalla ambaye alilihusisha tukio hilo na ushirikina alitoa rai kwa
wanakijiji kuacha vitendo hivyo kwa kuwa vinadhoofisha utendaji kazi wa
watumishi hususani walimu ambao si wazawa wa eneo hilo.
Aliongeza kuwa tabia hiyo ikizidi kuendelea
itasababisha walimu kuondoka ili kukimbia kupatwa na matatizo kama hayo ambayo
hayasaidii maendeleo ya kijiji chao.
Pia aliwasihi kuacha mara moja tabia hiyo ambapo
aliongeza kuwa mtu yoyote atakayebainika kuhusika na sakata hilo atahamishwa
kijijini hapo ambapo pia aliwataka wakazi waliohamia eneo hilo kinyemela
kujiandikisha ili kijiji kiwatambue.
Baadhi ya wanakijiji waliozungumza na waandishi
wa habari walionekana kushangazwa na vitendo hivyo ambapo walisema dunia ya
sasa ni tofauti na zamani ambayo walikuwa wakiamini kwenye ushirikina.
“ Mtu yeyote aliyekula nyama ya mwalimu huyu
airudishe la sivyo tukimuona nay eye atakiona cha moto lakini pia haya mambo
yalipitwa na wakati yalikuwa yakifanyika zamani bora wayaache” alisema Moses
Njeje mkazi wa kijiji cha Ruiwa.
Chifu wa eneo hilo Shadrick Melele alipotafutwa
kuzungumzia hali hilo amekemia vitendo hivyo ambapo pia amesema kuna mwanamke
ambaye anasadikiwa kuhusika na tukio hilo amejitokeza na kumwomba msaada chifu.
No comments:
Post a Comment