Tuesday, 4 June 2013

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA WAWASILI NCHINI TAYARI KWA MAZISHI


Umati wa waombolezaji ukijaribu kulikaribia jeneza la msanii huyo huku watu wngine wakijaribu kupiga picha wakati mwili wake ulipowasili kwenye uwanja wa JK Nyerere leo. 3 
Ukiingizwa kwenye gari. 4 
Wapiga picha wakipiga picha. 5 
P. Funk na wasanii wengine wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JK Nyerere 9Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwasili katika eneo hilo la mapokezi 10 
Ndugu na jamaaa wakiwa na majonzi huku wengine wakilia kwa uchungu. 11 
Hapa ni vilio tu wakimlilia Albert Mangwea 12 
Tipo na Bazo nao wameshiriki katika kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea 13 
Edwin Temba na Abraham Mosi nao walijumuika katika mapokezi hayo.


Mwili wa Msanii Albert Mangweha 'Ngwair' a.k.a mimi au Cow Boy uwewasili jijini Dar es Salaam hii leo majira ya saa 8 mchana na kupokelewa na maelfu ya mashabiki, wasanii wenzake, ndugu jamaa na marafiki.

Mwili huo uliokuwa umehifadhiwa katika sanduku zuri la kupendeza ulipokelewa na kuingizwa katika kagi maalum la kubebea maiti na safari ya Muhimbili ilianza huku waombolezaji wakilisukuma gari hilo wakielekea Hospitali ya Muhimbili ambako mwili utahifadhiwa hadi kesho utakapo pelekwa viwanja vya Lidaz kwa heshima za mwisho.

Wasanii maarufu wa Tanzania kutoka makundi mbalimbali ya muziki wa kizazi kipya walifika uwanjani hapo kuupokea mwili wa mwenzao.

Mangweha aliyezaliwa Novemba 15, 1982 na kufariki Mei 28, 2013 anataraji kuzikwa katika Manispaa ya Morogoro eneo la Kihonda nyumbani kwa mama yake

No comments: