Muonekano wa choo hicho kwa mbele kutokana na kukosa milango wamelazimika kutengeneza uzio wa nyasi.
Kushoto ndiyo tundu halisi la choo, na tundu la kulia limetokana na choo hicho kubomoka chenyewe.
Nyufa zilizomo kwenye kuta za choo hicho.
=============================
Na Edwin Moshi, Makete.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Uganga kata ya Luwumbu wilaya ya Makete mkoani
Njombe wapo hatarini kupoteza maisha yao kutokana na vyoo wanavyovitumia
kubomoka na kuweka nyufa na matundu makubwa kutokana na uchakavu.
Mtandao
huu umebisha hodi shuleni hapo hivi karibuni ka kukuta vyoo hivyo
vinavyotumiwa na wanafunzi vikiwa katika hali mbaya huku wanafunzi hao
wakiendelea kuvitumia bila wasiwasi.
Mwanafunzi
mmoja anayesoma darasa la tano katika shule hiyo ambaye hakupenda jina
lake liandikwe mtandaoni amesema haoni shida kutumia vyoo hivyo kwa kuwa
hakuna sehemu nyingine ya kujisaidia na kuongeza kuwa licha ya hatari
ya kupoteza maisha waliyonayo wanafunzi wanaotumia vyoo hivyo lakini
bado wataendelea kuvitumia.
Akizungumzia
suala hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo Eliuda Danie Kyando amekiri
kuwepo kwa vyoo hivyo chakavu na kusema kuwa ameshapeleka kwenye ngazi
husika suala hilo ambapo amejibiwa kuwa litafanyiwa kazi.
Amesema
kwa hivi sasa wanamuomba Mungu isitokee hatari yoyote kwenye vyoo hivyo
katika kipindi hiki wanaposubiri wakubwa kulishughulikia suala hilo
kama walivyomuahidi ingawa ni muda mrefu umepita.
"Mimi
katika taarifa zangu wakati mwingine huwa naandika kuwa shule haina
vyoo vya wanafunzi kutokana na uchakavu hebu ona mwenyewe vyoo gani
hivi, hii si hatari tupu, matundu mengine tumeziba na magogo ili
wanafunzi wasiingie" alisema.
Shule hiyo ambayo inadhaniwa kuanza miaka ya 1970 inakabiliwa na changamoto lukuki ikwemo majengo kwa kuwa mengi yamechakaa.
No comments:
Post a Comment